Na. Hassan Maabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema serikali imefuta kodi ya pango la ardhi katika majengo na maeneo yote ya taasisi ambazo zinatoa huduma katika jamii bila kufanya biashara na kuzalishi faida. 


Waziri Lukuvi amesema hayo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya wakazi wa jiji la arusha ambapo ametoa agizo kwa maafisa wote wanaohusika na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi kuziondoa katika orodha ya madeni taasisi binafsi, za dini, za serikali na mashirika yote ambayo hayazalishi faida.

Hata hivyo waziri Lukuvi amesema kwamba sheria hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 julai 2018 ambapo Serikali kupitia Bunge imeridhia kuondolewa kodi ya pango la ardhi taasisi za elimu, shule za msingi, sekondari, vyuo, vituo vya afya, hospitali, taasisi za umma na taasisi za dini kama misikiti na makanisa ambayo yalikuwa yanalipa kodi hiyo.

Pamoja na msamaha huo wa kodi Waziri Lukuvi amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri kote nchini kupima maneo yanayotoa huduma kwa jamii ili kuitambua mipaka ya shule, zahanati na maeneo mengine na kuzipatia hati miliki za ardhi zitakazo wawezesha kutambua mipaka ya maeneo hayo lakini taasisi hizo hazitalipa kodi tena.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jery Muro alipotembelea jiji la Arusha kwa ajili ya utatuzi wa migogoro ya ardhi. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea wakati wa mkutano na wakazi wa jiji la Arusha, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Fabian na kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu jiji la Arusha. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa jiji la Arusha wakati wa mkutano wa utatuzi wa migogoro ya ardhi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...