UONGOZI wa Viwanja vya Ndege vya Songwe na Kigoma, umejiandaa kwa kushirikiana na maafisa afya, kuhakikisha hakuna mgonjwa mwenye dalili za Ebola anaingia nchini, akitokea maeneo ya Tunduma na nchini Burundi.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Pius Kazeze alimwambia Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi.Bahati Mollel kwa njia ya simu kuwa, tayari Maafisa wa Afya wameshafunga mashine maalum (thermo scanners) inayotambua joto la mwili la abiria ambaye anasafiri kwa kupitia kiwanja hicho, na likizidi 38 anatakiwa kutoa taarifa za afya yake.

Bw. Kazeze amesema Kiwanja cha Songwe ni tofauti kidogo na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo zaidi wanakagua abiria wanaoondoka kwa kuwa wengi wanatoka mpakani maeneo ya Tunduma na kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Tayari maafisa Afya wamefunga mashine ya ukaguzi wa afya eneo la nje la kuondokea abiria kwani kwetu huku tunapata abiria wengi wanaotoka nchi jirani wanaopitia mpakani Tunduma, hivyo wengi wao wanatoka nchi zinazopakana na Kongo, ambayo inasadikika ugonjwa wa Ebola umeibuka kwa kasi kubwa,” alisema Bw. Kazeze.

Hatahivyo, amesema mbali na mashine hiyo kubwa iliyowekwa sehemu maalum, pia wanamashine mbili ndogo zinazotumiwa kwa kushikwa mkononi na maafisa Afya, lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Watumishi wa afya, ambao tayari wameshaomba kuongezewa mmoja ili kufanikisha kazi hiyo kuwa rahisi.
Mmoja wa abiria akikaguliwa na mashine ya mkono, iliyoshikwa na Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke, ikiwa ni moja ya njia za kudhibiti wagonjwa wa Ebola wasiingie nchini. Ugonjwa huo umetangazwa hivi karibuni kusambaa nchini Kongo.
Afisa Afya wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Peter Maseke (katikati) akikagua hati za kusafiria za mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Dar es Salaam, ambapo (kulia) ni mashine maalum inayotambua abiria wenye homa kali, ambayo ni moja ya dalili za ugonjwa wa Ebola.
Abiria wakiwa katika eneo la nje la kuondoka kwenye Kiwanja cha Ndege cha Songwe


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...