Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

STAR Media (T) Ltd, imewaomba radhi wateja wake pendwa na umma kwa ujumla kwa kutopata chaneli za bure kwa muda sasa.

Taarifa iliyotolewa  na Mkurugenzi Mtendaji Star Media(T)Wang Xiaobo amesema leo kuwa hiyo imesababishwa na kukosekana kwa elimu na mawasiliano mazuri kuhusu aina ya tofauti za dikoda (ving’amuzi) tulizonazo, ambayo yamesababisha kwa wateja wao kuendelea kulipia chaneli za bure.

"Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa ziko aina mbili za dikoda, ya kwanza ni ile ya Chaneli za bure (FTA) ambayo mteja halazimiki kila mwezi ili kutazama chaneli za bure.

"Na nyingine ni ya chaneli za kulipia, ambayo mteja atatakiwa kulipia kifurushi chake kila mwezi," amesema

Ameongeza kwa wateja wapya, dikoda (ving’amuzi) hizo zinapatikana kwenye maduka yao pamoja na mawakala wao, lakini kwa wateja ambao tayari wameshanunua dikoda (ving’amuzi) za kulipia wanaweza kubadilisha dikoda (ving’amuzi) zao kuwa FTA kwa kutembelea katika ofisi zetu na kupata utaratibu.
 Amesisitiza Star Media (T) Ltd, itaendelea kuzingatia masharti yote ya leseni, pia inaufahamisha umma kwamba imekubali kufuata na kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwamo kulipa faini ambayo tayari imeshaanza.

Pia wanawafahamisha umma wa watanzania kwamba sasa wanaweza kuendelea kufurahia chaneli za bure na huduma zetu kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...