Josephine Arnold Wakili wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA akifungua semina ya matekelezo ya Mradi wenye lengo la kuchangia ongezeko la ushiriki na uwakilishi wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na shughuli za kisiasa kwa ujumla wake 

Moja ya Shughuli ndani ya mradi huo ni pamoja na kumiarisha uwezo wa vikundi / Majukwaa ya wanawake katika ngazi ya wilaya za mkoa wa Dar es salaam ili waweze kuongelea changamoto zinazowazuia kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kisiasa, Walioshiriki katika semina hiyo ni vikundi na majukwaa ya wanawake katika ngazi za kata na wilaya za mkoa wa dar es salaam. Semina hiyo imefanyika kwenye hoteli ya New Africa leo.
Isabella Nchimbi Mwanasheria wa Chama cha Wawanasheria Wanawake akitoa mada katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Josephine Arnold Wakili wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA na Bi. Sara Kinyaga wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Mwezeshaji wa Semina hiyo Sara Kinyaga akitoa mada katika semiha hiyo
Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...