Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
TUZO mbalimbali za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017-2018 zimetolewa leo mjini Monaco nchini Ufaransa.

Katika tuzo hizo, Tuzo ya Golikipa Bora wa mwaka imekwenda kwa Kipa namba moja wa Real Madrid, Keylor Navas, kabla yakutolewa kwa Navas, tuzo hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Kipa wa Juventus anayechezea PSG kwa sasa, Gianluigi Buffon.

Nafasi ya Kiungo Bora, tuzo hiyo imenyakuliwa na Kiungo wa Kimataifa wa Croatia anayekipiga na Real Madrid, Luka Modrić.

Tuzo ya Mshambuliaji Bora imenyakuliwa na Mshambuliaji Matata wa Juventus aliyekuwa Real Madrid, Cristian Ronaldo.

Luka Modrić amewabwaga Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo na Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa UEFA.

Katika hafla hiyo, Nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid ameshinda tuzo maalum ya Rais wa UEFA 2018. 

Katika sherehe hiyo, Makundi mbalimbali yamepangwa kwa timu mbalimbali 3kuchuana katika msimu ujao wa Michuano hiyo ya Ligi ya 

Mabingwa Ulaya:-
Group A: Atletico Madrid, Dortmund, Monaco, Club Brugge;
Group B: Barcelona, Tottenham, PSV, Inter Milan;
Group C: PSG, Napoli, Liverpool, Red Star Belgrade;
Group D: Lokomotiv Moscow, FC Porto, Schalke 04, Galatasaray;
Group E: Bayern Munich, Benfica, Ajax, AEK Athens;
Group F: Manchester City, Shakhtar Donetsk, Lyon, Hoffenheim;
Group G: Real Madrid, Roma, CSKA Moscow, Viktoria Plzen;
Group H: Juventus, Man United, Valencia, Young Boys

Michezo ya hatua ya Makundi itaanza kupigwa Septemba 18-19 hadi Desemba 11-12 ambapo timu mbili kila Kundi zitaingia hatua ya mtoano itakayoanza kutimua vumbi February 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...