Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BARAZA la Michezo la Taifa limetangaza uchaguzi mkuu wa Chama cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) utakaotarajiwa kufanyika oktoba 06 mwaka huu katika Jiji la Dodoma.

Akizungumzia uchaguzi huo, Afisa habari wa BMT Najaha Bakari amesema kuwa fomu za uchaguzi zimeanza kutolewa katika ofisi za baraza hilo kuanzia leo hadi Oktoba Mosi mwaka huu.

Najaha amesema kuwa usaili utafanyika Oktoba 05 kuanzia saa 3 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na wajumbe sita wa kuchaguliwa.

Najaha amesema sifa za wagombea hao ni lazima wawe  na elimu ya kidato cha nne au zaifi, taaluma na uongozi katika mchezo wa baiskeli, awe raia wa Tanzania, awe na nidhamu pamoja na asiwe na historia ya kukutwa na hatia ya kufungwa zaidi ya miezi sita.

BMT imetoa wito kwa wenye nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo huu, waone umuhimu wa kuchukua fomu na kugombea nafasi stahili ili kuendeleza chama cha michezo huu pamoja na kuiletea sifa nchi.

Mbali na hilo Najaha amewasihi viongozi wa vyama vya michezo kuona umuhimu wa kuwa na ofisi zao kwani kuanzia sasa hivi Baraza halitalifumbia macho suala hilo kwa kuona vyama havina ofisi wala hawajulikani wanapatikana wapi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...