Na Stanslaus Makendi, Mahakama Kuu Dodoma.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imeanza mpango wa uanzishaji wa huduma za Kimahakama katika Wilaya zisizo na huduma hizo kwa sasa.Viongozi wa Mahakama katika Kanda hii wameanza kufuatilia na kukutana na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na Chamwino ili kupata maeneo ambayo yatatumika na Mahakama za Wilaya katika kipindi ambacho mpango wa kujenga Mahakama za Wilaya katika maeneo hayo unafanyiwa kazi.

Utekelezaji huu unafuatia agizo la Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya kufanya jitihada ya kuwa na Mahakama hizo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.Katika mazungumzo waliyofanya katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ilibainika kuwa huduma ya Kimahakama inahitajika sana kwa sasa katika eneo hilo kutokana na umbali mrefu uliopo kufikia eneo ambalo huduma za Mahakama ya Wilaya inapatikana kwa sasa (Kondoa).

Baada ya mazungumzo hayo viongozi wote wa pande mbili walitembelea na kuona eneo ambalo Ofisi ya Mkurugenzi imetenga kwa ajili ya matumizi ya Mahakama na Taasisi nyingine muhimu ambazo hazipo kwa sasa katika Wilaya hiyo.

Sambamba na hilo, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino nao walionesha uhitaji mkubwa wa uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya katika eneo hilo na wameahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha huduma hiyo inaanzishwa mapema katika Wilaya hiyo. 
 Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Bi. Maria Francis Itala ( wa pili kushoto) akiwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Zahara Muhidin Michuzi kufuatilia upatikanaji wa majengo kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
2 (33)
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na Hakimu Mkazi Mfawidhi (M) wakitoka katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kwenda kuona eneo lililopendekezwa kwa ajili ya uanzishaji wa Mahakama ya Wilaya pamoja na kuoneshwa kiwanja cha Mahakama katika Wilaya hiyo.
4 (18)
Muonekano wa nje wa jengo lililopendekezwa kwa ajili ya Mahakama ya Wilaya ya Chemba.
6 (7)
Muonekano wa jengo linalotumika kwa sasa na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa ambayo inatoa huduma za kimahakama kwa Wilaya ya Kondoa na Chemba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...