Helikopta iliyowasili kumchukua Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala akipatiwa matibabu mkoani Manyara

Na Said Mwishehe,

Globu ya Jamii.
PIGO kubwa Wizara ya Malialisi na Utalii! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya kutoke ajali ya gari aliyokuwa akisafiria Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamis Kigwangala ambayo imesababisha kifo cha Ofisa Habari wa Wizara hiyo, Hamza Temba (RiP).
Katika ajali hiyo ya gari kulikuwa na watu sita akiwamo Waziri Kigwangala ambaye ameumia katika mbavu, mkono na shingo na kwa sasa anapatiwa matibabu wilayani Manyara wakati wanaandaa utaratibu wa kumhamishia yeye pamoja na majeruhi wengine katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.
Akizungumza kwa njia ya simu asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema Waziri Dk.Kigwangala alikuwa anatokea mkoani Arusha kuelekea mkoani Dodoma na alipofika eneo hilo gari yao ikatapa ajali hiyo.
Amefafanua kwa sasa ndio yupo njiani anaelekea eneo ambalo ajali imetokea lakini kwa mujibu wa wasaidizi wake ni kwamba ajal hiyo imesababisha kifo cha mwandishi wa Waziri Kigwangala.
Alipoulizwa chanzo cha ajali hiyo Kamanda Senga amesema taarifa alizonazo ni kwamba eneo hilo kuna hifadhi ya wanyama na hivyo wakati gari ya Waziri inapita kulikuwa na mnyama barabarani na hivyo dereva akawa anajaribu kumkwepa.
"Wakati anamkwepa ndipo gari ilipomshinda dereva na kusababisha kupoteza muelekeo na hivyo kupinduka na kusababisha kifo cha mwandishi huyo na wengine kujeruhiwa akiwamo Waziri Kigwangala ambaye anapatiwa matibabu pamoja na dereva wake.
"Nikifika eneo la tukio nitakuwa na nafasi nzuri ya kutaja majina ya waliokuwamo kwenye gari hilo na hali zao kiafya. Lakini hadi sasa tunazo taarifa za kifo cha mtu mmoja ambaye ni mwandishi wa Waziri,"amesema Kamanda Senga.
Pichani juu na chini ni Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangwallah ambaye amepata ajali asubuhi hii akitokea Arusha katika eneo la msitu kabla ya kijiji cha Magugu maarufu kama Mguu wa Mjerumani ama Mdori. Kwa mujibu wa mbunge wa Mbulu vijijini Mhe. Flatei Massay alieleza kuwa mtu moja ambaye ni mwandishi wa habari amepoteza maisha. Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni Twiga aliyekuwa anakatisha barabara mbele yao na katika kumkwepa gari likapinduka.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...