Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limesema kuwa uchaguzi mkuu wa chama cha mchezo wa kuogelea Tanzania (TSA) ulienda vizuri ingawa kulikuwa na changamoto zilizojitokeza hapo awali.
Uchaguzi huo uliofanyika mapema wiki hii, uliweza kuwapata viongozi wapya watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne ambao wameapa tayari kwa ajili ya kuanza kutumikia nafasi zao kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo.
Akizungumzia uchaguzi huo Ofisa habari wa BMT Najaha Baklari amesema kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa amani kubwa sana ingawa awali kulitokea changamoto mbalimbali na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Juma Ikangaa aliweza kutoa rai kwa wagombea wote walioshinda nafasi zao wakazitumikie kwa ueweledi mkubwa ili kuleta manufaa kwa chama hicho, pia hata wale ambao hawakupata nafasi wae dele kuunga mkono.
Amesema kuwa uchaguzi ulikuwa na ushindani mkubwa sana hususani katika nafasi za Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu ambapo zilikuwa na wagombea zaidi ya mmoja na nafasi nyingine kuwa na mgombea mmoja mmoja lakini hakukuwa na wakati mgumu sana katika nafasi ya mwenyekiti, Mweka Hazina na Mkugenzi wa Elimu na Maendeleo ambazo zilikuwa na mgombea mmoja mmoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...