Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifungua mkutano wa wadau (hawapo pichani) wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika kwa siku mbili mjini Morogoro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu
Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Christina Hape akitoa ufafanuzi wa utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu.
Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu akiongea na wajumbe (hawapo pichani) katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifuatiwa na Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape.
Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu akiongea na wajumbe (hawapo pichani) katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu.
Washiriki wa Mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wakichukua dondoo muhimu wakati wa mkutano.
Afisa Sheria wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Deogratias Haule akitoa maelezo katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika mjini Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...