Wakazi
wa kijiji cha Timbolo,Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, wamepongeza
jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha mawasiliano
kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za
Mawasiliano ya uhakika jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli
za kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho hususani huduma jumuishi za
fedha(financial inclusion).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya uhakika.
‘’Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata huduma za kifedha,kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Kivuyo.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho katika kata ya Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo wamesema,imekuwa rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma pesa kwenda mtandao huo.
“ Kwakweli ukiwa na huduma za Haloteli,unafurahia kupata muda wa maongezi wa kutosha,data ndiyo siwezi kuelezea,yaani ni huduma rafiki sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema,Rehema Joshua,mkazi kijiji cha Timbolo,kata ya Sambasha,Wilaya ya Arumeru,mkoa wa Arusha.
“Sisi kama wananchi wa Timbolo tunashukuru kwanza kabisa jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya Halotel kuweza kuweka minara ya mawasiliano katika kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za mawasiliano katika maeneo yao na kusaidia wananchi kutumia huduma za mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya mawasiliano ya uhakika.,”
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda (katikati), akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo namna ya kutumia huduma za mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea miundombinu ya kampuni hiyo. 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel Kivuyo, akifafanua jambo wakati kwa waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Timbolo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha DC, Samwel Kivuyo, akifafanua jambo wakati kwa waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho kuangalia miundombinu ya mawasiliano iliyowekwa na Kampuni ya Halotel. Kushoto ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Josephine Mhina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...