Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
WATU wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiriwa na shtaka la kukutwa na nyara za serikali ambazo ni pembe mbili tembo zenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 34.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Hassan Mgaza maarufu kama Dingi na Daud Aniset almaarufu Mwambambe.

Mbele ya Hakimu Mkazi  Mwandamizi Salum Ally, imedaiwa, Agosti 18, 2018 katika eneo la ufukwe wa Bahari  katika Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa walikutwa na pembe mbili za meno ya tembo zenye thamani ya  USD 15,000 ambazo ni sawa na Sh. 34,275,000. Imedaiwa kuwa, nyara hizo ni mali ya serikali ambazo washtakiwa wanadaiwa kuwa nazo bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mkurugenzi wa wanyamapori.
Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa, mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ispokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Septemba 14.2018 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
 Watu wawili wakiwawamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kukutwa na nyara za serikali jijini Dar es Salaam leo. 
Watuhumiwa wakitoka katika mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...