WILAYA ya Manyoni mkoani Singida imetenga zaidi ya ekari 5000 kwenye Kijiji cha Masigati kwa ajili ya kupanda mikorosho mipya baada ya wananchi kuhamasisha kupanda zao hilo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa wakati wa ziara ya viongozi wa bodi ya korosho nchini ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini ambao yalifanyiwa utafiti na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho.

Viongozi wa bodi hiyo ambao walifika kwenye shamba la mfano lililopo katika Kijiji cha Masigati kwenye Halmashauri ya Manyoni ambalo lilianza mwaka jana ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba na Afisa Uhusiano Bryson Mshana wakiwa kwenye uhamasishaji wa kilimo hicho kwenye maeneo mapya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kati ya hizo ekari zilizopandwa ni 1250 kwa msimu uliopita wa kilimo na msimu umekaribia mwezi Desemba mwaka huu wataanza tena kuendelea na upandaji wa mikorosho mipya.

“Pamoja na kwamba tumetenga ekari 5,000 kwa ajili ya kulima kilimo cha Korosho lakini mipango yetu ni kufikia ekari 10,000 alisema pamoja na hayo tutaendelea kufanya uhamasishaji kwa wananchi kuweza kuchangamkia fursa ya zao hili na kupanda mikorosho kwa wingi “Alisema.
Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya ya kutembelea maeneo mapya yanayolima korosho nchini yaliyofanyiwa utafiti  na kubainika yanaweza kustawi zao hilo na hivyo uhamasishaji wa kilimo hicho ukafanyika akielezia mikakati ya wilaya yake kupanda zaidi ya ekari 5000 za mikoroshoMkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi kushoto akimsikiliza kwa umakini Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana wakati wa ziara ya viongozi wa bodi kuhamasiha kilimo cha zao la Korosho kwenye maeneo mapyaAfisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho nchini Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Afisa Kilimo ,Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Fadhili Chimsala Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Charles Fussi wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo na viongozi wa bodi ya Korosho mara baada ya kumalizia mazungumzo nayo kushoto ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na kulia ni Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...