Na. Vero Ignatus  Ngorongoro
OXFAM kwa kushirikiana na Shirika la PALISEP wameendesha mafunzo ya teknolojia ya kidigitali kwa wananchi wilaya ya  Ngorongoro mkoani Arusha ili kuleta  maendeleo katika jamii husika. 
Maratibu wa Teknolojia kwa maendeleo shirika la Oxfam Bill Marwa amesema  wametoa mafunzo kwa wananchi zaidi ya (90)yakiwa na lengo la wao kutambua namna ya kuitumia mitandao hiyo pamoja  nyenzo mbalimbali za kidigital kwa kutuma ujumbe mfupi, kutoa taarifa kwa viongozi wao wa kijiji,kujibuwa changamoto wanazokutana nazo kwaajili ya kujiletea maendeleo.
 "Kadri miaka inavyoenda kumekuwa na ongezeko la mitandao ya kijamii ulimwenguni hivyo Oxfam kama shirika limeona upo umuhimu wa maendeleo, kupata taarifa, kutoa matokeo"alisema Bill Marwa.Washiriki wa mafunzo hayo walifundishwa sheria za mtandao 2015 pamoja na makosa ya mtandaoni, jinsi ya kutumia vifaa hivyo katika namna ambayo havivunji sheria ya nchi. 
Sambamba na hayo walifundishwa maswala Mbalimbali jinsi ya ukingi haswa kwa wanawake kulinda haki za mwanamke na kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao.Mafunzo hayo yaliyokuwa ya siku nne yaliyoshirikisha kata zaidi ya 10 katika wilaya ya Ngorongoro,ikiwa ni mradi wa  miaka miwili unaotekelezwa katika mikoa (4) Arusha, Geita,Kigoma,na Mtwara katika wilaya za Mtwara vijijini, Mbogwe Geita, Kibondo,na Ngorongoro. 

Mradi huo unalengo la kuwawezesha wananchi kutumia nyenzo za digitali ili kujiletea maendeleo katika jamii husika,amabapo ulianzishwa rasmi mwaka 2016 desemba na unatarajiwa kumalizika novemba 2018 ,mradi huo upo chini ya ufadhili kutoka nchini Ubelijiji. 
Meneja wa Program Shirika la Oxfam Kefar Mbogela akitoa Elimu namna ya kutumia mitandao na nyenzo mbalimbali za kidigitali bila kuleta madhara kwa jamii wala kuvunja sheria ya mitandao hiyo
Rachel yeye anasema mwanzoni alikuwa akitumia simu ya hali ya chini ambayo alikuwa hapati mambo mengi ya faida ,ila kwa sasa mara baada ya kupewa simu na Oxfam imemsaidia sana kuweza kuwasiliana na na jamii ,amesema kwasasa anaweza kupaza sauti kwa kutumia simu yake,kutatua changamoto mbalimbali na viongozi wanapoona ujumbe wake wanatatua tatizo na majibu yanapatikana kwa wakati.
Darasa la mafunzo ya kutumia nyenzo za mitandao ya kijamii na namna ya kutumia nyenzo za kidigitali yakiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...