WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe.
January Makamba amesema Ofisi yake inaangalia uwezekano wa kutangaza
Ziwa Singidani na Ziwa Kindai katika Halmashauri ya Singida kama maeneo
lindwa kimazingira kwa kuwa yako hatarini kutoweka.
Waziri Makamba ameyasema hayo hii leo Mkoani Singida ikiwa ni siku ya
kwanza ya ziara yake katika Mikoa 9 hapa nchini yenye lengo kukagua,
kutathmini na kuzungumza na viongozi, wataalam, watendaji na wananchi
kuhusu maeneo yanayopendekezwa kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria ya
Mazingira kifungu namba 51.
Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mara baada ya kutoa tangazo hilo
katika gazeti la Serikali matumizi sahihi ya maziwa hayo yataainishwa ikiwa nipamoja na kupanda miti rafiki kuzunguka maeneo yote na kuzingatia makatazo yatakayotolewa.
“Ziwa Singidani liko hatarini kutoweka kutona na shughuli za kibinadamu,
hivyo kwa kutumia Sheria ya Mazingira nitashauriana na wataalamu wangu
kuona namna bora ya kunusuru maziwa haya ikiwa ni pamoja na
kuyatangaza kwenye gazeti la Serikali kama maeneo lindwa kimazingira.”
Makamba alisisitiza.
Imebainika kuwa, lengo la kuainisha na kutangaza maeneo hayo ni kulinda
mifumo muhimu ya kiikolojia (ikiwemo vyanzo vya maji, mito, maziwa,
mabwawa, milima na vilima, chemichemi, ardhi oevu, mazalia ya samaki na
misitu) ambayo hayana ulinzi wa Sheria nyingine.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua vifungu vya Sheria ya Mazingira mbele ya Watendaji na Viongozi wa Mkoa wa Singida juu ya maeneo lindwa. Wengine katika picha ni viongozi wa Mkoa wa Singida wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijionea uharibifu wa mazingira katika Ziwa Singidani ambao unatokana na shughuli za kibinadamu. Waziri Makamba ameazimia kunusuru Ziwa hilo pamoja na vyanzo vyake. Wengine katika picha ni viongozi kutoka Manispaa ya Singida.
Ziwa Singidani ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na shughuli zisizo endelevu za kibinadamu. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi ya kukagua na kuona namna bora ya kunusuru Ziwa hilo pamoja na mengine kwa mustakabali wa nchi yetu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...