Mkuu wa wilaya ya Arusha, Bwana Gabriel Dapharo (kushoto) akimkabidhi msanii Vanessa Mdee (kulia) tuzo ya kumshukuru kutoka kwa Shule ya Arusha girls kwa msaada wake na kujitolea kwake kwenye hafla ya makabidhiano ambapo kampuni ya nishati ya jua ya Off Grid Electric kushirikiana na Vanessa Mdee wametoa msaada wa mitambo nane ya nishati ya jua kwa shule hiyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kupata mwanga wa kuaminika wakati wa kujisomea nyakati za usiku.
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Bwana Gabriel Dapharo (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya nishati ya jua ya Off Grid Electric nchini Tanzania, Erick Donasian (kulia) tuzo ya kumshukuru kutoka kwa Shule ya Arusha girls kwa msaada kwenye hafla ya makabidhiano ambapo Off Grid Electric kushirikiana na Vanessa Mdee wametoa msaada wa mitambo nane ya nishati ya jua kwa shule hiyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kupata mwanga wa kuaminika wakati wa kujisomea nyakati za usiku.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya nishati ya jua ya Off Grid Electric nchini Tanzania, Erick Donasian (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Bwana Gabriel Dapharo (wa sita kulia), Mwalimu wa shule ya Arusha Girls, Mwasiti Kinyau (wa nane kulia), Msanii wa muziki Vanessa Mdee (watano kulia) na wanafunzi wa shule hiyo baada kampuni hiyo ya nishati ya jua kukabidhi mitambo nane kwa shule hiyo.

KAMPUNI ya nishati ya jua ya Off Grid Electric imetoa msaada wa mitambo nane ya ZOLA kwa shule ya Arusha Girls baada ya ombi kutoka kwa msaani maarufu Tanzania - Vanessa Mdee. 

Erick Donasian, Mkurugenzi Mtendaji wa Off Grid Electric nchini Tanzania alisema: "Tunalenga kutoa bidhaa na huduma za daraja la kwanza kwa wateja wetu kila siku, na pia kusaidia biashara na elimu nchini Tanzania. Kuthibitisha hili, tumeiongeza Arusha Girls school kwenye orodha ya shule 58 ambazo tumeziwezesha kufurahia mwanga wa kuaminika, salama, na huduma mashuhuri ambayo inapatikana pamoja na mitambo ya Off Grid Electric tu. Kupata fursa ya kuliwezesha ombi la Vanessa ilikua ni heshima na wajibu kwetu; tunafurahia kuchangia katika ustawi wa wanafunzi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla."

Vanessa Mdee aliongezea kwa kusema “Kama balozi wa shule ya Arusha Girls, ni wajibu wangu kutoa kilicho bora kwa ajili ya ustawi wa wasichana pale ninapoweza. Waliponiomba kuwasaidia waweze kusoma bila usumbufu wa kukatikiwa na umeme nyakati za usiku, ilikuwa ni wajibu wangu kutafuta mtoa huduma ya nishati ya jua aliye tayari kulitatua tatizo lao. Ninajivunia kumpata Off Grid Electric ambae ni mshirika wa kuaminika katika mpango huu na pia ni mshirikia mwenye kujali ustawi wa elimu."


Wanafunzi wa Arusha Girls wanafurahia faida zote za huduma za Off Grid Electric ikiwa ni pamoja na chanzo cha mwanga wa kuaminika na wa muda mrefu zaidi wakati wa kujisomea nyakati za usiku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...