Na Bashir Yakub
Sio siri wengi waliowekeza kwenye biashara ya bajaji,bodaboda,taxi na hata daladala wamejuta kufanya hivyo. Wengi wameingia hasara na mambo hayakuwa kama walivyotarajia. Na niamini,waliomo leo kwenye hiyo biashara sio wale walioanza, bali ni wageni kwani walioanza walishaacha siku nyingi kuepuka kichwa kuuma.
Sasa yafaa tuzingatie mambo kadhaa ya kisheria ili kuona namna gani unaweza kudhibiti biashara hii na hata ikikushinda isikushinde ukiwa mwenye kupoteza(looser).Katika kufanya hivyo tutizama mambo mawili, kwanza Mkataba, na pili Udhamini.
1.MKATABA.
Eneo la mkataba au makubaliano ni eneo muhimu sana tangu unapowaza biashara hii. Mkataba ndiyo tafsiri ya uhusiano wako na huyo unayemkabidhi chombo. Popote, na wakati wowote mtakapotofautiana rejea yenu ya kwanza ni mkataba. Mkataba ndio biashara yenyewe, na hivyo uimara wa mkataba utatambulisha uimara wa biashara, halikadhalika udhaifu wa mkataba huenda ukawa ndio udhaifu wa biashara.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...