Na Shani Amanzi,

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi Bodi ya Pamba Tanzania Ndg.James Shimbe amesema wakulima wakiweka kipaumbele kulima zao la pamba litaleta kipato kikubwa kwa Taifa kwani zao la Pamba nje ya nchi linauzwa kwa 80% na 20% ndani ya nchi ambapo mahitaji makubwa yanaenda Viwandani. 
 

Shimbe aliyazungumza hayo alipokuwa kwenye Kikao kazi cha Baraza la Madiwani tarehe 31/9/2018 kama mgeni mualikwa kuelezea zao la Pamba linavyoweza kulimwa katika wilaya ya Chemba kwa kuwa ardhi iliyopo inafaa kwa kilimo hicho.

Aidha Shimbe amesema “nchi yetu inapata mapato makubwa kwa kuuza pamba nje ya nchi katika nchi za China, India, Pakistan na Indonesia na tunapaswa kuuza kwa wingi katika Viwanda vyetu ili vitengeneze nguo na kuepuka nchi kuagiza nguo za mitumba nje ya nchi kama ilivyo sasa ”.
Shimbe amesema, uzalishaji wa pamba kwa ekari moja ni kilo 560-912 katika mikoa ya Iringa, Manyara,Tanga,Singida ,Katavi,Geita ,Mwanza, Shinyanga na tunapaswa kuzidi kuwahimiza wakulima wetu walime pamba kwa wingi kwani Pamba ni dhahabu nyeupe inayohitajika kwa wingi zaidi katika soko la dunia.

“Katika utafiti tulioufanya katika wilaya ya Chemba kilimo cha pamba tutaanza kuwawezesha wakulima wa kata ya kidoka, gwandi,Lahoda, na mrijo kwa kuwapatia pembejeo za kilimo cha pamba na msimo wa kilimo unaanza mwezi wa novemba 2018 na mvuno ni mwezi wa aprili, 2018”. Alisema Ndg. Shimbe.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amewapongeza wageni kutoka bodi ya Pamba kwa kuja wilayani Chemba na ameahidi watashirikiana na Wataalam wa kilimo, Wahe. Madiwani na Wananchi ili kuweza kurahisisha kuwaelimisha wakulima umuhimu wa zao la pamba ili kuwainua .

“Tunaelewa katika kilimo kunachangamoto ikiwemo uwezo mdogo wa vyama vya ushirika,mabadiliko ya tabia nchi,kuwepo Maafisa ugani wachache ,wakulima kutozingatia kanuni bora za kilimo na mtazamo hasi wa zao la pamba lakini nawaahidi tutajitahidi kukabiliana nazo ili uzalishaji wa zao la pamba uwe tegemeo kubwa kama ilivyo zao la alizeti”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...