Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika kujitambulisha leo Ikulu Mjini Zanzibar akifuatana na ujumbe wake.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesema kuwa Kenya na Zanzibar zinauhusiano wa kihistoria hivyo ushirikiano katika
sekta ya biashara kati ya pande mbili hizo utakuza uchumi na kuuendeleza udugu wa
damu uliopo.
Dk. Shein aliyasema hayo leo, Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi
mpya wa Kenya katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dan Kazungu aliyefika Ikulu kwa
ajili ya kujitambulisha.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Kazungu kuwa Zanzibar na Kenya zina
uhusiano na ushirikiano wa kihistoria hasa katika sekta ya biashara ambapo Zanzibar ilikuwa
ndio kitovu kikuu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki tokea karne ya 19.
Dk. Shein alieleza kuwa kuna kila sababu ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya
Zanzibar na Kenya katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ambapo kwa upande wa
sekta ya biashara ndio sekta pekee yenye historia kati ya pande mbili hizo.
Alisema kuwa wananchi wa Kenya na Zanzibar wana udugu wa damu na kutokana na matukio
kadhaa ya kihistoria yakiwemo Watawala waliozitawala nchi hizo yamejenga ukaribu mkubwa
na kumpelekea Dk. Shein kusisitiza haja ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kenya Nchini Tanzania Mhe.Dan Kazungu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambilisha akiwa na ujumbe wake (hawapo pichani).
Katika maelezo yake, Rais Dk. Shein aliunga mkono wazo la Balozi huyo wa Kenya la kuwekwa
utaratibu maalum wa kuzidisha ushirikiano huo katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya
biashara kati ya Kenya na Zanzibar kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua ustawi wa maisha ya
wananchi wa pande mbili hizo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...