*Azungumzia dawa za viwandani zinavyotumika kama dawa za kulevya

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amesema matumizi ya dawa za kulevya nchini yamepungua kwa asilimia 90 huku akieleza kuwepo kwa mbinu mpya ambapo dawa za viwandani zimeanza kutumiwa na baadhi ya watu kama sehemu dawa za kulevya.


Hivyo amesema ipo haja ya kuhakikisha kunakuwa na mikakati mipya ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya huku akiomba wakuu wa vyombo vinavyohusika na kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya barani Afrika kuweka mikakati ya kuiabiliana na mbinu mbalimbali ambazo zinatumiwa na wanaofanya biashara hiyo.

Waziri Mkuu amesema hayo leo baada ya kufungua mkutano wa 28 wa wakuu wa vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi za Afrika ujulikanao kama (28th HONLEA- Afrika), jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC),ambao unashirikisha wajumbe zaidi ya 120 kutoka nchi 54 za Afrika.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza ipo haja kwa nchi hizo kuangalia kwa namna gani wanaweza kuweka mikakati ya kukomesha biashara ya dawa za kulevya.
Ameeleza namna ambavyo baada ya kufanikiwa kudhibitiwa kwa dawa za kulevya wapo baadhi ya watu wasiwaaminifu ambao wanachukua dawa zinazotengenezwa viwandani kama sehemu ya dawa za kulevya.


Ametoa mfano wa dawa hizo ni pamoja na dawa za usingizi ."Zipo dawa zinazotengenezwa viwandani watu wasiowaaminifu wanazichukua na kisha kuzibadilishia matumizi kuwa dawa za kulevya,"amesema.

Hivyo amesema lengo la  mkutano huo ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi hizo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo Vinavyopambana na Biashara ya Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC)  jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Bibi Jo Dedeyne ambaye ni  Katibu Mkuu Kiongozi wa Taasisi za  Umoja wa Mataifa zinazoshughulikia dawa za kulevya na uhalifu (United Nations Office on Drugs na Crime - UNODC)  baada ya kufungua Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na Dawa za Kulevya   kutoka nchi za Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 17, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...