Maadhimisho ya Juma la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Maonesho ya wadau wa jeshi hilo yamefungwa leo Dodoma, ambapo msisitizo ulikuwa ni kwa watanzania kushiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa kufunga ving'amuamoto viwandani.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akisindikizwa na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenda kutembelea mabanda ya wadau wakati wa maazimisho ya Juma la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, akioneshwa kifaa mahsusi kiitwacho "king'amua moto" kitumikacho kugundua moto ukiwa hatua za awali na kuwezesha kukabiliwa kwa urahisi wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akipata maelezo ya namna ya utoaji wa huduma mbalimbali za kiuhamiaji mbalimbali toka kwa Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji, Alice Mhoja wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakionesha namna ya kuokoa mtu aliyenaswa katika jengo refu.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala akipata maelezo ya namna ya kutumia zana mbalimbali zinazotumika kuzima mioto ya aina tofauti toka kwa Luteni Kalalawina wakati akitembelea mabanda ya wadau wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwenye maonesho yaliyoandaliwa sambamba na maazimisho ya Juma la Jeshi hilo yalifanyika katika uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...