Na Profesa Joseph Mbele

Nilisafiri tarehe 15 Julai mwaka huu kutoka Marekani kwenda Tanzania. Nilishukia Nairobi, kwa shughuli binafsi, ikiwemo kununua vitabu vya ki-Swahili. Kitabu nilichotamani zaidi ni Sauti ya Dhiki cha Abdilatif Abdalla ambacho nilitaka kukisoma kwa makini kuliko nilivyowahi kufanya kabla. Ninawazia pia kutafsiri kwa ki-Ingereza baadhi ya mashairi.

Nilivyoingia tu katika duka la vitabu la Textbbook Center, Kijabe Street, nilikitafuta kitabu cha Sauti ya Dhiki. Nilikiona, kikiwa na jalada tofauti na lile la mwaka 1973. Nilinunua pia Kichwamaji, Kaptula la Marx, na Dhifa, vya Euphrace Kezilahabi; Mashetani, tamthilia ya Ebrahim Hussein, na Haini, cha Adam Shafi.
Tangu zamani, nimekuwa na baadhi ya vitabu vya Kezilahabi, Ebrahim Hussein, na Adam Shafi. Ninafurahi kujipatia vile ambavyo sikuwa navyo. Hata hivi, nimegundua kuwa sasa nina nakala mbili za Mashetani na mbili za Kichwamaji. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...