NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa, ameingilia kati mgogoro wa ardhi kati ya kampuni ya Mohammed Enterprises na kijiji cha Zumba ,Mpiji Stesheni ,Soga na Kipangege huku akimuomba Waziri mwenye dhamana kutatua mgogoro huo.

Aidha ,amelazimika kuunda kamati ndogo ya watu 12 ,itakayofuatilia jambo hilo ili haki itendeke .

Akizungumza na wananchi hao ,Jumaa alisema, ifikie hatua ya wataalamu na viongozi wenye dhamana kukutana na wananchi ,kuwaeleza jitihada zinazochukuliwa na serikali kutatua malalamiko yao bila kukaa kimya .

"Tatizo hili nimelikuta ,katika kipindi changu ni miaka saba sasa ,2015 niliongea na waziri na kuja na kamati ya ardhi ,na kutolewa maelekezo mbalimbali lakini bahati mbaya ,wakati wa uchaguzi ule waziri husika hakuweza kufika "

"Mkuu wa wilaya ya Kibaha aliwahi kufika kuongea na wananchi ,na mkoa wa Pwani ulifikishiwa hatua zinazochukuliwa walitumwa wataalamu kufanya tathmini na kujua mapungufu ya ardhi ya wananchi wanayohitaji ." alisema Jumaa.

Jumaa alieleza ,tangu hapo hakuna taarifa ya hatua hizo zilipofikia lakini amejipanga kufuatilia suala hilo kwa kushirikiana na kamati iliyoundwa .

"Mh Lukuvi ni mwelewa na ana hekima , naamini atalitatua tatizo hili bila kuangalia upande wowote ,ili kuondoa dhana ya wananchi kuwa mwekezaji kaiweka serikali mfukoni " alifafanua Jumaa.


Hata hivyo ,Jumaa alikemea tabia inayofanywa na meneja wa mwekezaji huyo aitwae Mndeme kunyanyasa baadhi ya wananchi na wengine kupigwa na kupelekwa polisi bila hatia .
 Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ,akizungumza na wananchi kijiji cha Zumba kuhusiana na mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na kampuni ya Mohammed Enterprises.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mpiji Stesheni ,Saidi Abdallah akizungumza katika mkutano na wananchi kuelezea mgogoro wa ardhi.
 (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...