MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kukamilika kwa Flyover ya
Mfugale iliyopo Tazara kutasaidia kunusuru ndoa za watu wa mkoa huo.
Makonda
amesema hayo leo mbele ya Rais Dk.John Magufuli wakati wa uzinduzi wa
Flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam
ambapo amesema kwamba kukamilika kwa Flyover hiyo ni wazi sasa wananchi
wanaondokana na changamoto ya foleni kubwa.
"Kuna
ndoa za watu zimeingia kwenye kutoaminiana kwa sababu tu ya msongamano
wa magari makutano ya Tazara.Wapo waliokuwa wanachelewa kurudi nyumbani
na wakiulizwa na wenza wao wanasingizia foleni.
"
Kuna baadhi yao walikuwa wanatumia foleni ya Tazara kama kificho kwani
wanakwenda gesti na wakiulizwa wanasema walikuwa kwenye foleni,"amesema
Makonda na kuongeza kwamba
"Sasa
kuanza kutumika kwa flyover hii kutaimarisha ndoa kwani hakutakuwa na
visingizio tena,"amesema Makonda huku akitumia nafasi hiyo kufikisha
salamu za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa Rais.
Pia
amesema flyover hiyo itarahisisha shughuli za kiuchumi kwa mkoa wa Dar
es Salaam ambapo ameeleza kufurahishwa kwake na namna ambavyo Rais
Magufuli amedhamiria kuboresha maisha ya wananchi na hiyo imesababisha
Watanzania kutembea kifua mbele.
Makonda
ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Magufuli ameendelea
kuboresha miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam kwani kuna barabara
nyingi ujenzi unaendelea.Amesema kuna miradi mingi ya maendeleo ambayo inaendelea kujengwa ambapo amesema kuna kilometa chache ambazo zimesalia.
Makonda
amesema kutokana na kazi kubwa ambayo inaendelea kufanyika wananchi wa
Mkoa wa Dar es Salaam ombi lao ni moja tu ambalo ni Rais kufanya ziara
katika mkoa huo.
"Nafikisha
ujumbe wa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ni kwamba wanatamani
kukuona ukipita kwenye mitaa yao na hivyo kiu na hamu yao ni kukuomba
ufanye ziara ili uwatembelee nao wakuone",amesema Makonda.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japan(JICA)nchini Tanzania Toshio
Nagase amesema kukamilika kwa Flyover ya Mfugale kutasaidia kuboresha
maisha ya watu wa Dar es Salaam na nchi jirani.
Pia
amesema awali ukitaka kwenda Uwanja wa Ndege walikuwa wanaondoka mapema
katikati ya Jiji kwa sababu ya makutano ya Tazara lakini sasa wanaweza
kuchelewa kuondoka kwa sababu ya daraja la juu la Mfugale
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...