MWENGE wa uhuru umepokelewa Mkoani Manyara ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya sh15.7 bilioni kwenye Halmashauri saba za mkoa huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akizungumza jana wakati wa kupokea mwenge huo kutoka Mkoani Arusha alisema utatembea miradi mbalimbali ya maendeleo, kwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi. 

Mnyeti alisema gharama ya miradi ya halmashauri ya wilaya ya Babati ni sh3.490 bilioni, Babati mji sh1. bilioni, Mbulu Mji sh1.1 bilioni, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu sh3.4 bilioni, Hanang sh1.5 bilioni, Kiteto sh6.9 bilioni na Simanjiro sh1.1 bilioni.

"Tunawakaribisha kwenye mkoa wa Manyara ambapo wananchi wana hamu kubwa ya kuona mwenge wa uhuru na kusikiliza ujumbe wa elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu," alisema Mnyeti. 

Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu alisema kwenye halmashauri ya Wilaya hiyo mwenge wa uhuru utatembea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.4. 

Kitundu alisema mwenge wa uhuru utaweka jiwe la msingi kituo cha afya Nkaiti, bweni la wavulana shule ya msingi Mbugwe na kupanda miti ya kumbukumbu.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kaimu mkuu wa Mkoa wa Arusha. Ukiwa mkoani Manyara mwenge wa uhuru utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisoma taarifa ya mkoa huo baada ya kupokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoani Arusha, ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7 kulia kwake ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho.  
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2018 Charles Kabeho akisoma jiwe la msingi la bweni la shule ya sekondari Mbugwe, Wilayani Babati, baada ya kuizindua, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Elizabeth Kitundu. 
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Elizabeth Kitundu akipanda kwenye ukiwa katika halmashauri ya Wilaya ya hiyo mwenge wa uhuru umetembelea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.490.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu mwenge wa uhuru baada ya kupokea kutoka Mkoani Arusha eneo la Minjingu madiwani. 
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...