Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha taarifa mbalimbali za hospitali wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma, kulia kwake ni katibu wa afya wa hospitali hiyo Mwanaisha Hassan.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kuhakikisha mashine ya kutolea huduma za X-ray  inafanya kazi ndani ya siku 14. 

Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kuangalia na kujiridhisha na hali ya utoaji huduma za afya  katika Hospitali hiyo leo jijini Dodoma. 

"Ifikapo Septemba 21 nataka kuona mashine ya kutolea huduma za X-ray na vifaa vingne viwe tayari kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma na maeneo yanayoizunguka kwani Hospitali hii ni tegemezi kwa wakazi wa mkoa huu la sivyo hatua stahiki zitachukuliwa bila ya kumuonea mtu haya" alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha,Dkt. Ndugulile ametoa siku 30 kwa uongozi wa hospitali hiyo kukarabati jengo la bima ya afya baada ya kukagua na kutoridhishwa na muonekano wake kwani linaleta kero kwa wateja wanaokwenda kupata huduma Hospitalini hapo. 

Mbali na hayo Dkt.  Ndugulile ameonekana kukerwa na uzembe  wa watendaji wa Hospitali  hiyo na kusababisha kuwakemea vikali na kuhaidi maagizo aliyoyatoa yasipotekelezwa kwa wakati hatua za kinidhamu zitakuchululiwa kwa vitendo.

Wakati huo huo dkt.Ndugulile ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuwarudishia fedha wagonjwa walizotumia kununua dawa pamoja na sindano kwenye maduka yaliopo nje ya hospitali hiyo ilihali wana vifaa hivyo  takribani ya kutosha miezi sita kwenye stoo yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikagua maboksi ya sindano katika stoo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wagonjwa waliokua wanasubiri huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...