Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma

IKIWA msimu wa kununua mazao umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia ubora wa mahindi.

Aidha, amesema nchi inachakula cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.

" Haiwezekani NFRA itumia fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..

Aliongeza: “Lazima chakula tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe taswira ya NFRA kwa sababu awali kulikuwa na tatizo la chakula kuharibika kwa kipindi kifupi.”

Zikankuba alisema ili kuhakikisha mahindi ya wakulima yanaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa NFRA tayari imekwishatoa elimu kwa wakulima kupitia vikundi na kwenye vyombo vya habari.Alibainisha kuwa baada ya elimu hiyo wakala umefanikiwa ambapo wakulima kutoka maeneo ya Makambako, Sumbawanga na Mpanda wameanza kuzalisha na kuuza mahindi yenye ubora kwa NFRA.

“Changamoto iliyopo ni kwa baadhi ya wakulima wachache ambao bado wamekuwa wagumu kubadilika na wale ambao wanaamini wakitumia nafasi zao wanaweza kuuza mahindi yasiyo na ubora,"Alisema kwa mkulima kuwa na mahindi yenye ubora unatoakiwa utasaidia katika kupata soko la NFRA, pia katika taasisi zingine zinazonunua nafaka hiyo za ndani na nje ya nchi.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...