*Yatangaza kuanzia mwaka huu vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kupatiwa elimu ya ufundi bure

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewashukuru Watanzania kwa namna ambavyo wameendelea kukiamini huku kikieleza mambo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.John Magufuli watu wanaona na ndio siri ya ushindi wao.

Pia kimetangaza kwamba kuanzia mwaka huu vijana wenye kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 watapatiwa elimu ya ufundi bure na hiyo  ni fursa kwa vijana.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humphrey Polepole wakati anatoa sababu za ushindi wa kishindo ambao Chama hicho wameupata katika uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga ,Monduli pamoja na Kata zote ambazo uchaguzi mdogo umefanyika.

Kuhusu kuaminiwa Polepole amesema kutokana na mambo makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais Dk.John Magufuli wananchi wanaona na ndio maana kimeendelea kuaminika na kupata ushindi wa kishindo"Yanayofanyika ndani ya nchi yetu watu wanaona.Tumeshinda Jimbo la Ukonga na Monduli.Tumeshinda Kata 23 na kati ya hizo 12 tumepita bila kupingwa.

"Siri ya kuendelea kuaminika na kushinda chaguzi ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi madhubuti wa Rais.Dk.John Magufuli," amesema Polepole.Amefafanua kwamba unapozungumzia kupita bila kupingwa kuna sababu mbalimbali na kwamba uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na hasa sheria za uchaguzi.

"Hivyo wanaoshiriki chaguzi wanatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi na kinyume na hapo unapoteza sifa," amesema.Akifafanua zaidi kuwa wanaojiita wapinzani kwa sasa wamebaki na siasa za kubeza mazuri yanayofanyika.Polepole ameeleza pamoja na mambo makubwa yanayofanyika ya kimaendeleo CCM pia imetoa maagizo na maelekezo  kwa mawaziri kushughulika na shida za Watanzania.nakwamba ni marufuku kwa viongozi kujifungia maofisini badala yake watoke kwenda kutatua kero za watu huko waliko.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...