KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ametembelea na kufanyamazungumzo na watendaji wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA)jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kikao  na Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Domina Msonge akitoa taarifa fupiya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018 mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kutembelea ofisi zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa  walipotembelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo jijini Dar es Salaam na kumsomea taarifa ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Domina Msonge (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa taarifa fupi ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa kwa 2017/2018 mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo kutembelea ofisi zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko, biashara naMahusiano wa Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa, Egwaga Nungu
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amewashauri wahandisi nchini kujenga utamaduni wa kuandaa mipango ya miradi ya maendeleo ya maji na kuwa na majibu kabla ya kukutana na maswali ya viongozi wa kisiasa.

Profesa Kitila ametoa ushauri huo leo wakati akiwasilisha mada yake inayohusu maendeleo ya maji kwa wahandisi ambao wapo katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa Bodi ya Usajili Wahandisi wa Tanzania (ERB) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

Hivyo wakati anatoa mada hiyo pamoja na mambo mengine amewaambia iwapo watakuwa na mipango inayoonesha gharama za miradi mbalimbali inayotekelezwa itakuwa rahisi kujibu maswali ya viongozi wa kisiasa bila kuchelewa badala ya kusubiri kuulizwa.

"Wahandisi wengi wamekuwa wakisubiri maelekezo kutoka kwa wanasiasa hali ambayo inachelewesha maendeleo ya miradi ya maji hasa vijijini.Ni vema wahandisi wakawa mbele kwa.majibu na hiyo itawezekana kwa kuwa na mipango endelevu," amesema.

Ameongeza kuwa "Wahandisi wanatakiwa kuwa mbele ya wanasiasa kwa kuwa mipango ya maendeleo na hasa miradi ya maji ili kuepuka maelekezo ambayo sio ya kitaalamu," amesisiza na kueleza maji na maendeleo na maendeleo na maji.

Prof.Kitila amewasisitiza wahandisi nchini kiwa ili miradi ya maji kuwa na tija wana kila sababu ya kuwa wabunifu kwa kubuni miradi mipya na kubwa ni kutatua changamoto zilizopo .

"Ni wajibu wa wahandisi kuhakikisha wanabuni miradi ya maji,kwa mfano wanaweza kubuni mradi wa maji wa kuondoa changamoto Singida kwa kutumia maji yaliyopo Ziwa Victoria," amesema.

Amefafanua  kwa kufanya  hivyo hata akitokea kiongozi akazungumzia utatuzi wa maji mkoani Singida tayari wahandisi walishakuwa na majibu na kinachobaki ni utekelezaji.
  
Kuhusu mikakati ya Serikali katika sekta ya maji nchini, Profesa Mkumbo amesema kuna mpango wa miaka mitano ambao utagharimu zaidi ya Sh.Tril 10.4 kwa lengo la kufanikisha upatikanaji wa maji.

Akizungumzia kiasi cha maji kilichopo nchini Profesa Mkumbo Kuhusu kiasi cha maji kilichopo Kitila alisema hali bado ni nzuri ambapo pamoja maji kupungua Tanzania ina ujazo wa trilioni 92.

Pia ametoa mwito kwa kila mwananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo huku akiwasisitiza wahandisi kutambua dhamana walinayo katika maendeleo ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...