Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii
Kampeni za
udiwani kata ya Vingunguti Zimefungwa leo katika uwanja wa Msikate tamaa,
ambapo pole pole alikuwa mgeni rasmi na kuwaeleza Waliofika kwenye mkutano huo kuwa chama cha
Mapinduzi chini ya mwenyekiti wake Dkt John Pombe Magufuli kimefanikiwa mambo mengi ya maendeleo ambapo hata wapinzani wamekosa hoja za
msingi.
"Watu wenye akili zao vijana na kama
Kumbilamoto na akinamama mtatiro wameona Mazuri ya CCM na kuamua kumuunga mkono
Rais, nami na waaomba kesho siku ya
jumapili tarehe16/2018 wakazi wa Vingunguti mpigieni kura Omary Said
Kumbilamoto mapematu tuwetumeshinda Jina lake kwenye karatasi litakuwa
nambambili"amesema
Viongozi wengine waliomwombea kura Kumbilamoto
ni pamoja na mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu , Bonna Kaluwa, wa Segerea,
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es salaam Frank Kamugisha na
Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM akitokea CUF
na Wenyeviti saba wa Mitaa ya kata hiyo.
Katika hatua
nyingine Diwani wa kata ya Buguruni kwa mnyamani Shukuru Dege leo amejivua
uanchama wa Chama cha wananchi CUF na kujiunga na CCM, ambapo amesema ameamua
kujiunga na CCM kwa kuwa CUF imepoteza mwelekeo na pia ameamua kuunga mkono
serikali ya awamu ya tano.
Pamoja na
hayo Mgombea wa kata hiyo Omary Said Kumbilamoto amesema amefurahishwa na
wananchi wa kata hiyo kwa kumuunga mkono na kuwaomba tena kesho kumpigia kura
kwa wingi iliaendeleekuwatumikia akiwa
CCM na kuwaletea maendeleo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwisho wa Kampeni za Mwisho Udiwani kata ya Vingunguti
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa , Humphrey Polepole akimnadi mgombea wa Udiwani wa kata ya Vingunguti Kupitia CCM , Omary Kumbilamoto
Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Vingunuti Omary Kumbilamoto akiomba Kura kwa mara ya mwisho wakati w akuhitimisha kampeni
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kombo kupitia Chama Cha Wananchi CUF ,Sharifu Mbulu akizungumza mara baada ya kurejea CCM katika mkutano wa kufunga kampeni Vingunguti
Mbunge wa Segerea Bonnah Kaluwa akizungumza Jambo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika Mkutano wa kuhitimisha Kampeni Vingunguti
Aliyekuwa Diwani wa Mtoni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam , Benard Mwakyembe akizungumza wakati wa Mkutano wa kuhitimisha Kampeni kat aya Vingunguti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...