Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KATIBU Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo amewataka  wadau wa maji nchini kushiriki katika utoaji wa maoni kuhusiana na utungaji wa sheria mpya ya maji ili kuweza kudhibiti upotevu wa maji.

Amezungumza hayo katika Ofisi za Dawasa jijini Dar Es Salaam na kuongeza kuwa sheria hii mpya itasaidia Mambo mengi ikiwa ni pamoja na udhibiti wa maji ambayo yamekuwa yakipotea kwa asilimia 44 mpaka sasa

Prof Mkumbo amesema wizara inapendekeza kuanzishwa kwa Taasisi maalumu  ya kushughulikia miradi ya maji mijini na vijijini yaani Rural Water Agency, Taasisi ambayo imekusudia kuimarisha Jumuia za watumiaji wa maji kwa ngazi za vijiji na miji ikiwa ni pamoja na uimarishaji wa Taasisi mpya ya Dawasa

Kutunga kwa sheria hii mpya ya maji kutaongeza matamanio kwa watumiaji wa maji na kuhakikisha kila Mtanzania anapata maji safi na salama kwa uhakika  zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya DAWASA Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja amewataka wananchi wa Dar Es Salaam na Pwani kushirikiana na Dawasa katika ufanyaji kazi wake hasa kutoa taarifa punde inapobainika uvujaji wa maji, na kusisitiza kuhusu utungaji wa sheria mpya unapofanyika wananchi watoe maoni ili mchakato uwe na tija kwani sheria hii ina manufaa makubwa kwa wananchi.
Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Menejiment mpya ya Mamlaka ya Maji Taka na Maji Safi (DAWASA) inayoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) leo baada ya kukutana nao ofizi za DAWASA Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...