![]() |
Waziri wa maji na umwaguliaji profesa Makame Mbarawa |
Na Agness Francis,Globu ya jamii.
WAZIRI wa maji na umwaguliaji profesa Makame Mbarawa amewata wakazi waliojenga na wanaoishi Katika miundombinu ya mabomba ya maji hapa nchini kuondoka maramoja.
Profesa Mabrawa amesema hivyo ili kuweka usalama kwa wananchi hao kuondokana na adha ya kuhatarisha maisha ya wananchi hao.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuwa mwananchi atakaekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kwa kuwaondoa wote waliojenga katika miundo mbinu hiyo, kwa kuwa sheria iko wazi na inajulikana
Aidha Waziri Mbarawa amesema kuwa serikali ya Tanzania kupitia shirika LA maji safi na maji taka Dawasa itahakikisha zoezi hilo linafanikiwa katika kuhakikisha wananchi hao wanafata maagizo hayo bila kukiuka.
Hata hivyo Mbarawa amewataka wananchi wote kuwa waangalifu katika kuzuia upotevu wa maji ambapo amesema mpaka kufika 2020 tatizo a maji litakwisha na huduma ya upatikaniani wa maji itainhezeka u kuwafikia wanachi wote wa mijini na vijijini.
Ambapo ameahidi kubadilisha utendaji wa kazi hasa katika utekelezwaji wa wakandarasi wasio na vigezo vya ufanyaji kazi kwa ufanisi pamoja na wasimamizi kulega lega katika usimamizi wa majukumu yao.
Vile vile profesa Mbarawa amezungumzia utungwaji wa Sheria Mpya ya maji kuwa italeta mapinduzi ya upatukanaji wa huduma ya maji nchini kote kwa urahisi.
"Wanachi wote wanaruhusiwa kutoa maoni yao kuhusu sheria hiyo mpya itakayotungwa,kwa Kuwa sheria hiyo haitakuwa ni yakwangu bali ni ya sisi wote"amesema profesa Mbarawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...