NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MKUU wa mkoa wa Iringa amepiga
marufuku wafanyabiashara wadogo wadogo kunyanyaswa katika mahali ambazo wanafanyia
biashara kwa kuwa wanatoa kodi ambayo inachochea kuleta maendeleo ya watanzania
hususani mkoani iringa tukielekea kuijenga Iringa mpya.
Akizungumza kwenye mkutano
na wafanyabiasha wadogodogo wa manispaa ya Iringa mkuu wa mkoa Ally Hapi
alisema kuwa wafanyabiasha wadogo wadogo maarufu kama machinga wanatakiwa kufanya
biashara zao kwa kufuta taratibu na sheria za nchi huku viongozi wakiancha
kuwanyanyasa kwa kuwa nao ni wafanyabiashara.
“Toka nikiwa mkuu wa wilaya
najua umuhimu wafanyabiasha wadogo wadogo kwa kuchangia katika kukuza uchumi wa eneo husika hivyo natangaza rasmi
ni marufuku kuwanyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa” alisema
Hapi
Hapi aliwataka polisi
wanasimamia eneo lastand kuu kuacha mara moja kunyanyasa wafanyabiasha wadogo wadogo wanaofanyia biashara katika eneo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally
Hapi akiongea na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga wa
manispaa ya Iringa kwa lengo la kusikiliza kero na changamoto ambazo
wanakabiliana katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa na kuhakikisha
wanaijenga Iringa mpya ambayo inatakiwa na wanairinga
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo
wadogo maarufu kama machinga walijitokeza kumsikiliza mkuu wa mkoa wa
Iringa Ally Hapi na kama ambavyo unawaona walivyokuwa makini kumsikiliza
hapo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...