Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars"Stars inayodhaminiwa na bia ya Serengeti Premium Lager inatarajia kuondoka leo Alhamis Septemba 6,2018 saa 7 mchana kuelekea nchini Uganda kwa mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Afcon dhidi ya Uganda. 

Tutaondoka na kikosi cha wachezaji 23 na viongozi 7 watakaoambatana na viongozi mbalimbali wa TFF. 

Ni mchezo tunaokwenda kwa nia ya kufanya vizuri na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kundi letu.

Kufanya vizuri kwa timu hii ni fahari ya kila Mtanzania tuendelee kuiunga mkono timu hii inayokwenda kupeperusha bendera ya Tanzania. 

Kocha Emmanuel Amunike anasema anaendelea na maandalizi akiendelea kuangalia mapungufu mbalimbali na kuyafanyia kazi ambapo anaamini kikosi kilichopo huku wachezaji wanaocheza nje wakiwa wameripoti wote. 

Anasema kikosi kina muelekeo mzuri na maelekezo anayotoa anaona yanaeleweka. 

Nahodha Mbwana Samatta amesema mchezo huo utakuwa wa ushindani na kikubwa ni kufuata matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Kikosi kinachoondoka kwenda Uganda 

Aishi Manula (Simba), Salum Kimenya(Tz Prisons), Frank Domayo(Azam FC), Salum, Kihimbwa(Mtibwa), Kelvin Sabato(Mtibwa), David Mwantika(Azam FC) , Ally Abdulkarim(Lipuli), Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania ), Beno Kakolanya (Young Africans), Hassan Kessy (Nkana,Zambia), Gadiel Michael (Young Africans), Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini), Aggrey Morris (Azam FC), Andrew Vicent (Young Africans ), Himid Mao (Petrojet,Misri), Mudathir Yahya (Azam FC), Simon Msuva (Al Jadida,Morocco), Rashid Mandawa (BDF,Botswana), Farid Mussa (Tenerife,Hispania), Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium), Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan), Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania), Yahya zaydi(Azam FC)

kocha Mkuu Emmanuel Amunike na wasaidizi wake Hemed Morocco na Emeka Amadi,Mtunza Vifaa Ally Ruvu na madaktari wawili Richard Yomba na Gilbert Kigadya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...