Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akiongea na Viongozi na wananchi wa Nyang'wale.
Madiwani wa Nyang'wale wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea Halmashauri hiyo.

Watumishi sita pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Geita baada kubainika kuchezea fedha za miradi ya maendeleo zilizoelekezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale. 

Watu hao ni Aliyekuwa mkurugenzi wa Nyang'wale Calous, wahasibu Robert na Godson, Mweka Hazina Ronatus, Afisa habari Zahoro, Katibu wa Afya Alfred Joseph, na Afisa utumishi Muhando B.Mhando.

Wizi uliofanyika katika fedha za miradi ya Afya, Elimu, Jengo la Utawala, na Maji ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuna ubadhirifu wa Sh.Bilioni 2.2. 

Kushikiliwa kwa watumishi hao kumetokana na agizo alilolitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ambapo ameelekeza vyombo vya dola kufanya kazi yake na tayari wanashikiliwa na jeshi hilo. 

Jafo akiwa katika mkutano wa kikazi wilayani humo amevitaka vyombo vya Dola kusimamia vyema jambo hilo ili waliohusika mali zao zishikiliwe ili kufidia fedha zilizopotea sambamba na hatua zingine za kisheria. 

Hata hivyo Waziri Jafo amemtaka mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na Makamu wake kujitafakari kama wanafaa kusimamia fedha za wananchi wa Nyang'wale. 

Aidha Waziri Jafo amepongeza Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo Mariam Chaurembo kwa kubaini kwa haraka ubadhirifu huo wakati wa makabidhiano na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wa awali. 

Amewataka wakurugenzi nchini kuwa makini katika kusimamia majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...