Naibu waziri wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na waandishi wa haabri jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea eneo la viwanja vilivyonunuliwa na serikali kwaajili ya wananchi waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege, Richard Mayongela akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kutembelea Viwanja vilivyopo Luhanga Kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam na kukubali bila kinyongo kutekeleza agizo la  Naibu waziri wa Wizara ya UchukuziMhandisi Atashasta mara baada ya kutoa agizo hilo.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
TANZANIA Remix kuchukuliwa hatua za kisheria kulingana na mkataba unavyosema. Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelea viwanja vya fidia vya wananchi Waliopisha upanuzi wa Uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam.

 Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege  (TAA) Richard Mayongela amesema kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Tanzania Remix na zitatekelezwa bila kuogopa.

 Pia amesema kuwa "Tanzania Remix tumieni wiki hii moja mliyopewa kwaaajili ya kutekeleza agizo hilo la sivyo mtachukuliwa hatua za kisheria bila kuogopwa"

Pia amewaomba wananchi wawe wavumilivu kwani haki ya Mtu haiwezi kupotea bure ili wananchi waweze kufurahia matunda yao.

 Kiwango cha uvumilivu kwa mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) umefikia mwisho na sheria zitachukuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...