Na David Edward, VETA.
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule amesema kuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na uhitaji wa Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuwazesha wanannchi wa mkoa huo kupata ujuzi wa ufundi kwa maendeleo ya mkoa na Taifa kwa ujumla.
Dkt Halfan Haule aliyasema wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa katika hafla ya makabidhiano uliofanyika wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, amesema vijana wa Mkoa wa Rukwa ni fursa kupata mafunzo ya ujuzi na kuweza kujiajiri au kujiariwa.
Amesema wanaishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli kutatua tatizo upatikaji wa chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi mkoani humo.
Amesema vijana watapata ujuzi wa kusindika mazao mbalimbali na maendeleo yatapatikana kupitia usindikaji ambao utaogeza thamani ya mazao.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akizungumza katika Hafla ya
kukabidhiana eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu naMafunzo ya Ufundi Stadi
(VETA) Adelina Macha akitoa taarifa za kuhusiana na mipango ya ujenzi ya
Chuo cha VETA mkoani Rukwa.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt Halfan Haule akiwa katika picha ya pamoja na
watendaji wa VETA Kanda VETA Makao Makuu na Viongozi mbalimbali wa Mkoa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Soko la Ajira VETA, Hildergardis Bitegera akikabidhi
mchoro wa ramani ya Jengo la Chuo VETA Rukwa kwa Mkandarasi atakayejenga
Chuo hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...