Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANAFUNZI watatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamepata ufadhili kusoma mwaka wa tatu kwa kulipiwa ada kupitia kampuni ya Bima ya Metropolitan.

Akizungumza wakati wa kupokea hundi ya sh.milioni 4.5 Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Immanuel Mnzava amesema kuwa kampuni ya Bima ya Metropolitan kupitia Chama cha Mawakala wa Bima (TIBA) kimefanya jambo la kuigwa katika umuhimu wa kusaidia wanafunzi ambao wana uhitaji wa kuweza kuhitimu masomo yao.
Mnzava amesema kuwa sekta ya Bima inakua kwa kasi nchini hivyo lazima kuwepo na watalaam wa kutosha.

Wanafunzi waliopata ufadhili huo Paschalina Msofe,Rhoda Maholy pamoja na Leonard Mahimbo.

Amesema wanafunzi hao walikuwa na changamoto ya kiuchumi ambayo ingewafanya wakwame kuhitimu mwaka wa tatu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar amesema kuwa wanajibu wa kufanya hivyo bila kulazimishwa.

Amesema kuwa watu wakipewa elimu kunaongeza tija kwa serikali katika kuwa na watalaam wataosaidia maendeleo ya uchumi.

Aidha amesema waliofadhiliwa sio wakihitimu wakafanye kazi katika kampuni hiyo bali watafanya sehemu yeyote ikiwa nia kutoa huduma ya bima katika maendeleo ya nchi.

Mmoja wa wanafunzi waliofadhiliwa Paschalina Msofe amesema kuwa kazi yao ni kusoma bidii na kutoa matokeo mazuri kwa kile walichosome katika utoaji wa huduma ya bima nchini.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Immanuel Mnzava akizungumza wakati wa kupokea hundi ya wanafunzi waliofadhiliwa katika chuo hicho.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar akizungumza kuhusiana na kampuni hiyo kufadhili ada kwa wanafunzi.
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dkt. Immanuel Mnzava akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Metropolitan Suresh Kumar kwa ajili ya ada kwa wanafunzi kwa ada ya mwaka wa tatu.
 Mwanafunzi wa IFM Rhoda Maholy akitoa shukurani kwa niaba wanafunzi wenzake kuhusiana msaada kusoma mwaka wa tatu kwa ufadhili.
Wanafunzi wa IFM wakiwa na hundi ya mfano wa ada ya iliyotolewa na Kampuni ya Bima ya Metropolitan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...