Na Emmanuel Masaka,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake wilayani Mkuranga mkoani Pwani Mariam Ulega mwishoni mwa juma amekabidhi msaada wa kuku 4000 ambao watatolewa kwa wanawake wajasiriamali 400 ambao wamehudhuria mafunzo ya ujasiriamali.
Akizungumza wakati akikabidhi kuku hao kwa wajasirimali ,amesema kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla na amewataka wawe na ushirikiano ili wafiikie malengo yao.
Kwa upande wa baadhi ya akina mama hao wameshukuru kwa kupewa msaada huo na kuahidi kuwatunza kuku hao na kueleza kuwa kuku hao watakuwa chanzo cha miradi mikubwa zaidi.
Akiongea na Globu ya Jamii baada ya Mama Ulega kukabidhi vifaranga hao, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya AKM Glitters Company Limited, Bi. Elizabeth Swai, amesema amefurahishwa na juhudi zinazofanywa na Jukwaa la wanawake la Mkuranga na kwamba kwamba kampuni yake itaendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia wanawake hao kwa kutoa elimu ya namna ya kuendesha ufugaji bora wa kuku.
Bi. Swai, ambaye kampuni yake ndiyo iliyodhamini msaada huo, ameeleza kuwa AKM Glitters ni kampuni iliyojizatiti kukuza ufugaji wa kuku na ukulima wa kisasa kwa njia ya uzalishaji bora na matunzo.
Kampuni ya AKM Glitters inajishughulisha na ufugaji wa kuku aina ya Kuroiler, utotoaji wa vifaranga, utayarishaji wa chakula cha kuku na pia hutoa elimu ya ufugaji vijijini.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga, Mariam Ulega akizungumza na wanajasiriamali kuhusu kuwatunza kuku waliopewa ili kujiongezea kipato.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkuranga,Mariam Ulega akiwakangua kuku kabla ya kuwakabidh wananchi walilaya hiyo kwajili ya kufunga iliwaweze kujikwamua kiuchumi.
Mwenyekiti wa jukwaa la la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akiwakabidhi wananchi kuku 3000 kwa ajili ya kufunga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuongeza pato la Taifa, ambapo kila mwananchi alipewa kuku 10 (picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...