JOPO la Madaktari Bingwa wa MOI linalomhudumia Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla limemruhusu kutoka wodini baada ya kujiridhisha kwamba afya yake imetengamaa na anaweza kurejea nyumbani na atakuwa anakwenda hospitalini hapo  kama mgonjwa wa nje kwa ajili ya muendelezo wa matibabu yaliyosalia.

Jopo hilo la madaktari bingwa watano  wa kada za Mifupa, Usingizi na magonjwa ya ndani limefikia maamuzi hayo baada ya kumhudumia Dkt. Kigwangalla toka tarehe 12/08/2018 alipohamishiwa katika taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu ya kibingwa ya mkono wake wa kushoto baada ya kupata matibabu mengine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amemtakia kila kheri Dkt Kigwangalla katika kutekeleza majukumu yake ya kitaifa kwani ni muda muafaka wa kwenda kuwatumikia wananchi.
“Kwa niaba ya jumuiya ya Taasisi ya Mifupa MOI, tunakutakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yako ya ujenzi wa Taifa. 

Ilikuwa ni  heshima kubwa kuwa nawe hapa kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja... Tunaamini umeridhishwa na huduma zetu na kama kuna mahali umeona mapungufu ni vyema ukatujulisha ili turekebishe” alisema Dkt Boniface. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt.Respicious Boniface (kushoto) akizungumza jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa MOI Dkt.Respicious Boniface (kushoto) wakifurahia jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara alipokuwa amekwenda kumuaga. Kulia ni Mkuu wa Wod hiyo, Happyness Mligo 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiondoka hospitalini kwa furaha kubwa baada ya kuruhusiwa na madaktari.
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...