Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anataraji kufanya ziara ya kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi katika mikoa nane ya Tanzania bara katika wiki mbili kuanzia tarehe 17 hadi 30 Septemba 2018.

Ziara hii ni katika utekelezaji wa kampeni yake ya “Funguka kwa Waziri wa Ardhi” ambayo aliizindua rasmi mwezi Januari mwaka 2018 yenye lengo la kuzunguka nchi nzima kusikiliza migogoro na kero za wananchi zinanzohusu ardhi na kuzitafutia ufumbuzi papo hapo.

Katika wiki mbili hizi za kutatua migogoro ya ardhi katika mikoa nane waziri Lukuvi ameeleza kuwa kuanzia tarehe 17 hadi 19 atakuwa katika mkoa wa Mara katika wilaya ya Bunda, Musoma na Tarime na baadae tarehe 20 hadi 30 atakuwa katika mikoa ya Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Njombe, Iringa na Morogoro.

“Nipo njiani kuelekea mkoa wa Mara ambapo siku ya jumatatu tarehe 17 Septemba ntaanzia wilayani Bunda ili kutatua mgogoro wa Bibi Nyasasi Masike na kukagua kiwanja chake kama nilivyomuahidi Mheshimiwa Rais wakati alipofanya ziara yake wilayani Bunda na kunipigia simu moja kwa moja” Amesema Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akicheza na Wakazi wa kijiji cha Lolkisale Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua mgogoro mkubwa wa wakazi wa maeneo hayo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisoma mabango ya Wakazi wa kijiji cha Nafco Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipotembelea na kutatua migogoro mikubwa ya wakazi wa maeneo hayo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akivishwa mavazi ya heshima ya kimasai na Wakazi wa kijiji cha Eng’arooji Wilayani Monduli Mkoani Arusha alipofika kuwatatulia mgogoro wa ardhi uliokuwa umewagawa wananchi hao katika makundi mawili ambapo Waziri Lukuvi aliweza kutatua mgogoro huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...