Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

HII KAZI ITAFANYIKA: Hiyo ni kauli ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja wakati wa utambulisho wake baada ya kuteuliwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo.

DAWASA mpya, iliundwa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutoa kauli na kutaka DAWASCO na DAWASA ziwe kitu kimoja, agizo ambalo Wizara ya Maji na Umwagiliaji kama wasimamizi wa mamlaka hiyo kuunda DAWASA mpya itakayokuwa na bodi ya wakurugenzi moja.

Uteuzi wa kwanza wa Rais Dkt Magufuli ni wa Mwenyekiti wa Bodi Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na baadae kuteuliwa kwa bodi ya wakurugenzi iliyoundwa na wataalamu mbalimbali wa maji.

“Nimshukuru sana Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa uteuzi wake, ameniamini sana kwa kunipa majukumu haya makubwa kuongoza mkoa wa Dar es Saalaam na Pwani,” alianza kwa kusema.

Alisema, Mabadiliko haya ni mabadiliko ya kihistoria, kwa kuona hatua nyingine inapigwa kwa kutatua tatizo la umaskini, malazi na ujinga. Stadi mbalimbali zinaonesha huduma za maji zikiboreshwa kwa asilimia moja uchumi wa nchi huongezeka kwa asilimia nne na huduma zikizorota kwa asilimia moja uchumi hupungua kwa asilimia nne.

Ni kwelil; Kuna changamoto zinazowakabili DAWASA katika suala la upatikanaji wa maji pembezoni mwa mji, Kwa Mkoa wa Dar es Salaam ifikapo mwaka 2030 utakuwa ni moja ya majiji makubwa barani Afrika na ongezeko la watu litakuwa ni Milioni 11 na makadirio ya maji kwa siku yatakuwa ni n Lita Milioni Moja na Laki Moja (110,000).

Mhandisi Luhemeja ameweka mikakati mbalimbali ya DAWASA  baada ya kukabidhiwa dhamana ya kuiongoza Mamlaka hiyo na hatua ya kwanza ni kuhakikisha miradi iliyokuwa inasuasua inamalizika kwa wakati tena ndani ya siku 100.

Siku 100 za Mhandisi  Luhemeja ndani ya DAWASA, mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ameweza kumuahidi ndani ya siku 100 miradi ya maji iliyokuwa inasuasua na mingine kutokumalizika kwa wakati imepata dawa nayo ni uongozi mpya wa DAWASA.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa utambulisho wake kwa Menejimenti mpya iliyozinduliwa Septemba 09 Mwaka huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...