Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha huduma kwa wateja imetoa msaada wa vitu mbali mbali kwa kituo cha yatima cha Mgolole Orphanage Center, Morogoro.
Msaada huo ni pamoja na vitanda, neti, magodoro, deep freezer, chupa za chai, hot pot, sukari, sahani, sabuni, nepi, pampers na toy za watoto vyote vikiwa na thamani ya TZS 18 milioni.
Kutoa kwa msaada huo ni muendeleo wa kampuni ya Airtel Tanzania kupitia programu ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo kukubali kutoa sehemu ya mshahara wao ili kusaidi huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Akiongea mara baada ya kutoa msaada huo kwa kituo hicho cha Mgolole cha Morogoro, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba alisema muda mrefu wafanya kazi wa Airtel kupitia Airtel tunakujali imekuwa ikitembelea na kusaidia vituo mbali mbali vya yatima ikiwa ni pamoja na kuwapa misaada mbali mbali.
Leo ni siku yenye furaha sana kwetu zote kwani mayatima ni sehemu ya Jamii yetu na ni muhimu kuwapa upendo pamoja na kuwafariji. Hiki ambacho tumekuja kutoa leo hapa ni kidogo lakini nina uhakika kitagusa mioyo yenu lakini zaidi ni kujua tuko pamoja nanyi na tunawajali sana, alisema Lyamba.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba (kulia) akikabidhi msaada wa dogoro kwa Makamu Mama Mkuu wa kituo cha yatima cha Mgolole, Morogoro. Airtel Tanzania kupitia mradi wake wa Airtel Tunakujali walitembelea kituo hicho pamoja na kutoa msaada wa vitu mbali mbali vyenye dhamani ya TZS 18 milioni mwishoni mwa wiki. Kati kati ni Meneja wa Kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania Deogratius Hugo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...