Benki ya Azania yenye matawi yake sehemu mbali mbali nchini
imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja, lengo kuu likiwa ni kuwashukuru
wateja wake kwa kuwa nao bega kwa bega katika ukuaji wa benki hiyo.
Katika maadhimisho hayo benki ya Azania imewatembelea wateja kwenye
sehemu zao za kazi lengo likiwa ni kuona namna gani wanaweza kuboresha
huduma zao, mbali na hilo waliweza kutoa zawadi na vyeti kwa wateja wao
lengo likiwa ni kuwashukuru kwa kuichagua benki hiyo.
Baadhi ya wateja waliopatiwa Vyeti na Zawadi kwenye maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa mteja.
Benki ya Azania imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora kulingana na mahitaji yake.
Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa watoa huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...