Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Laurence Masha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Busega Raphael Chegeni na vijana wengine 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wakituhumiwa kufanya vurugu kwenye nyumba ya mwekezaji wa matunda ya Parachichi Peter Cruise na kutoa vyombo vyake nje kinyume cha taratibu.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya kosa hilo Oktoba 27 majira ya saa tatu asubuhi kwenye makazi ya mwekezaji yaliyopo katika eneo la Rungwe Mission na kuharibu mali hali iliyozua mabishano makali kabla jeshi la polisi kufika eneo la tukio na kuwakamata watuhumiwa ambao watafikishwa mahakama mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Masha na wenzake wanadaiwa kufika nyumbani kwa mwekezaji huyo kwa kuvunja mlango wa nyumba na kisha kutoa vyombo nje kwa nguvu/
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa watu hao japo kuwa amesema kuwa hana taarifa za ujio wao licha ya (watuhumiwa hao) kudai wanakwenda kutekeleza amri ya mahakama inayowapa uhalali wa kunmwondoa mwekezaji huyo kwenye makazi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...