Na Beatrice Lyimo - CHINA
MKURUGENZI wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ataendelea na ziara yake nchini China ambapo leo Ijumaa mchana atatembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari cha China na kutoa mhadhara.
Katika mkutano huo, moja ya masuala anayotarajia kuzungumza na wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho ni kuhusu diplomasia ya Tanzania na China iliyopelekea kuwa na ushirikiano wa karibu mpaka sasa.
Aidha, Dkt. Abbasi pia atazungumzia wajibu wa wanahabari na namna wanavyotakiwa kuenenda ili kutekeleza wajibu wao katika sekta nzima ya habari na mawasiliano.
Mbali na hayo, akiwa msimamizi wa sekta ya habari nchini Tanzania Dkt. Abbas katika mkutano huo ataeleza hali ya sekta ya habari Tanzania ilivyo sasa na ijayo kwa maendeleo ya nchi.
Dkt. Abbasi na ujumbe wake wa Maafisa Habari na Uhusiano Serikalini wapo mjini Beijing kwa ziara iliyolenga kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake wakipewa maelezo ya kiutendaji wa kazi za kila siku zinazofanywa na Shirika la Habari la CCTV na CGTN kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Shirika hilo mapema Jana jijini Beijing, China.
Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake alipotembelea vyombo vya habari vya CCTV na CGTN na China Redio Kimataifa Beijing China.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...