01:Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini (JET) John Chikoma akifafanua jambo kwenye semina semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya ya uhifadhi wa mazingira  na wanyamapori.Semina hiyo ilifanyika wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Baadhi ya washiriki wa semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori nchini Tanzania.Semina hiyo iliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET).
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) wakiwa pamoja na wadau wengine wakiwamo wafadhili miradi ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori pamoja na waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Sehemu ya waandishi wa habari za mazingira wakiwa kwenye moja ya semina iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira(JET).






*Mkurugenzi wa JET John Chikomo aelezea namna wanavyounga mkono 
juhudi za Serikali kwenye uhifadhi wa mazingira na kulinda wanyama


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Uhifadhi wa Mazingira nchini Tanzania(JET) kimekuwa chachu kubwa ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira nchini kupitia waandishi walioko ndani ya chama hicho.

Kupitia JET waaandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wamekuwa wakiandika habari zinazohusu uhifadhi wa mazingira na wanyama pori.Ni JET ambayo imeamua mara kwa mara kufanya semina za kuwajengea uwezo waandishi wa habari za mazingira kutambua nafasi yao katika kuelimisha jamii ya Watanzania umuhimu wa kutunza mazingira kwenye hifadhi zetu za taifa.

Kwangu naiona JET kama chombo muhimu katika kuhakikisha ufidhi wa mazingira unapewa kipaumbele.JET imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali katika kufahakikisha mazingira yanalindwa kikamilifu.

Kwa mwaka huu JET kupitia fedha za wafadhili imefanikiwa kutoa semina za aina mbalimbali kwa waaandishi wa chama hicho pamoja na wadau wengine.JET kupitia Mkurugenzi wake John Chikomo hakika imekuwa ikifanya kazi nzuri ya kusimamia uhifadhi wa mazingira nchini.

Kupitia semina hizo zinazoandaliwa na JET kumekuwa na mafunzo mbalimbali yanayozungumzia umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na kuyahifadhi.Ni semina ambazo pamoja na kuweka mikakati imekuwa ikikimbusha historia ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ndani ya nchi yetu ambayo kimsingi ilianza tangu enzi za Serikali ya Wakoloni.

Semina ambazo zinaeleza hatua kwa hatua namna ambavyo Taifa hili limekuwa likitunga sheria, kanuni na sera ambazo zitasaidia kusimamia utunzaji na uhifadhi wa mazingira ndani ya nchi yetu.

Nikiri JET imeamua kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.JET inaamini na kutambua fedha ambayo inapatikana kutokana na watalii wa ndani na nje kuja nchini kutembelea hifadhi zetu.JET inatambua fedha ambayo Serikali yetu inapata kutokana na watalii kuja nchini kutembelea hifadhi zetu kuangalia wanyama.

Hongereni JET kwa kazi ambayo mnaifanya .mmekuwa nguzo muhimu ya kuandaa waandishi wa habari za uhifadhi wa mazingira.Binafsi ni miongoni mwa waandishi wa habari ambao nimebahatika kushiriki semina za JET.Nimejifunza mambo mengi kuhusu uhifadhi.Nimejifunza kuhusu sheria za nchi yetu kwa maana ya faida na changamoto zake kwenye eneo la uhifadhi.

Katika semina iliyofanyika Oktoba mwaka huu wilayani Bagamoyo Mkurugenzi wa JET John Chikomo anasema wamekuwa wakishirikiana na wadau mbalimbali kuzungumzia masuala ya uhifadhi wa mazingira na kwamba kwa sasa wapo kwenye mradi wa miezi sita ambao unalenga waandishi wa habari kujengewa uwezo wa kuandika habari za mazingira.

"Mradi huu wa miezi sita umejikita zaidi kushughulikia uhifadhi wa mazingira na mbali ya kutoa mafunzo kwa waandishi pia tumekuwa tukitoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa taasisi mbalimbali.Tumekuwa tukitoa ruzuku kwa lengo la kujengea uwezo taasisi ambazo tunafanya nazo kazi za uhifadhi,"amesema Chikomo. 

Amefafanua kuwa JET inatambua juhudi za Serikali ya Awamu ya tano ambayo pamoja na mambo mengine ya kusimamia uhifadhi bado imekuwa na majukumu ya kuhamasisha watalii kuja nchini kutembelea hifadhi zetu."Ukweli ni kwamba JET tunaunga mkono kwa vitendo juhudi za Serikali kuhamasisha watalii kutembelea hifadhi zetu.Ndio maana mbali ya uhifadhi pia tunazungumzia umuhimu wa kutunza wanyama waliopo kwenye hifadhi zetu nchini," anasema Chikomo.

Pamoja na mambo mengine Chikomo anasema kuwa kimsingi JET kwa muda mrefu imeamua kujikita kwenye eneo hilo la uhifadhi na utunzaji wa mazingira na wanyamapori na wanajivunia kuwa sehemu ya kusimamia uhifadhi huo kupitia kalamu za waandishi wa habari za mazingira.

Baadhi ya watoa mada kwenye semina ya JET wanaelezea hatua kwa hatua namna ambavyo babu zetu walivyokuwa wanaishi na wanyama huku wakitumia sheria zao za asili kulinda wanyama na uhifadhi wa mazingira.Mmoja wa watoa mada Stanlaunce Nyembea anasema,pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali bado kanuni za asili za kulinda wanyama na mazingira kwenye baadhi ya maeneo zinatumika kama vile sehemu za misitu, samaki, ndege na mazingira yetu,". 

Amesema kuwa mbali ya mababu zetu kulinda wanyama na mazingira, baada ya kuja Waraabu ambao mbali ya kufanyabiashara ya binadamu pia walikuwa wanafanyabiashara ya kusafirisha pembe za ndovu.

"Baada ya kuondoka Waraabu wakaja Wajeruman ambao walipofika walikuta kuna mila ambazo zilitumika kulinda wanyama lakini waliona bado kuna haja ya kutengeneza sheria za kuhadhi na kulinda wanyama pori.Mwaka 1961 baada ya kupata uhuru ndipo zilipoanza pia kutungwa sheria zetu wenyewe,"amesema na kuongeza sasa mwaka 2009 ndio tukawa na sheria ua uhifadhi wa wanyama pori ila cha kukumbuka mwaka 2004 tayari kulikuwa na sheria ya mazingira.Sheria ya mazingira ina kanununi nyingi na moja wapo ni urari wa vizazi(usawa).Kanuni nyingine ni kinga ni bora kuliko tiba."

Kwa mujibu wa sheria za uhifadhi ni kwamba shughuli za kibinadamu haziruhusiwi kwenye maeneo ya hifadhi labda shughuli za madini.Hata hivyo sheria inaeleza wazi kuwa wananchi wanaruhusiwa kufanya shughuli rafiki katika kulinda wanyama na mazingira.

Itoshe kuelezea tu JET kupitia semina zake kwa waandishi wa habari zimekuwa na tija kwa nchi yetu ya Tanzania ambayo ni moja kati ya nchi chache duniani ambayo imaemua kuhifadhi misitu yake ambapo imehifadhi asilimia 32 ya ardhi yake yote.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa JET John Chikomo ni kwamba wao wataendelea na mikakati yao ya kuhakikisha jukumu la kuzungumzia umuhimu wa kulinda wanyama na kuhifadhi mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...