*Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar wafanya 
msako mkali kuhakikisha anapatikana

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuna Wazungu wawili wanasakwa kwa kuhusika kuratibu mpango wa kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji 'Mo'.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa taarifa za awali zinaonesha kwamba katika tukio hilo kuna wazungu wawili wanahusika kuratibu tukio la kutekwa kwa Mo Dewj.

"Tupo hapa kwa ajili ya kufuatilia tukio hili la kutekwa kwa Mo.Taarifa za awali ambazo tumezipata zinaonesha kuna Wazungu wawili wamehusika kuratibu tukio la Mo kutekwa."Tumeanza kufuatilia na wananchi wasiwe na wasiwasi,kikubwa watupe taarifa nasi tutazifanyia kazi," amesema Kamanda Mambosasa akiwa eneo la Hoteli ya Collessium  eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam ambako tukio la kutekwa Mo linadaiwa kutokea.

KAULI YA MAKONDA
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema taarifa za kutekwa kwa Mo zimeshutua wengi lakini anaamini atapatikana kwani tayari vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake.

Makonda amesema kuwa kikubwa wananchi wa Dar es Salaam kutokuwa na wasiwasi na wawe watulivu wakati vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea  kufuatilia.

HAJJ MANARA ATOA NENO
Wakati huo huo Msemaji wa Klabu ya Simba Hajj Manara amesema kikubwa ni kwa sasa ni utulivu na kuacha vyombo vya ulinzi vifanye kazi yake.

Pia amesema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu ni kumuomba ili Mo apatikane akiwa salama na anaamini atapatikana."Mbali ya kuwa Mo ni shabiki wa soka bado tukio la kutekwa kwake limeshutua makundi mbalimbali," amesema Manara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...