Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamefanikiwa kukamata kiwanda  cha kutengeneza Pombe kali ambacho kimekuwa kikizalisha bidhaa hiyo bila ya usajili.
Moja ya dira za serikali ya awamu ya tano ni kufikia uchumi wa kati kupitia Viwanda ,hata hivyo baadhi ya wafanyabiahara watafsiri Dira hii tofauti kwa kuamua kuanzisha Viwanda bila ya kufuata matakwa ya Sheria na taratibu za nchi.

Hali hii imejidhihirisha mkoani Kilimanjaro katika mji mdogo wa Himo baada ya Polisi,TRA na TFDA kubaini uwepo wa kiwanda bandia kinachozalisha Pombe kali .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamisi Issah amesema jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na idara nyingine za serikali kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana pamoja na kuhakiki ubora wa bidhaa kwa ajili ya afya ya watumiaji.
Zoezi la kubaini uwepo wa viwanda bandia katka mkoa wa Kilimanjaro ambapo katika siku za karibuni viwanda vilivyogundulika ni vile vinavyotengeneza Pombe za kienyeji na Pombe kali ,baadhi  vikiwa katika wilaya ya Rombo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamisi Issah akitizama baadhi ya chupa ambazo zimendaliwa kwa ajili ya kujaza kimiminika cha Pombe kali.
Sehemu ya Mitambo iliyopo ndani ya kiwanda hicho kilichopo katika wilaya ya Himo ambacho kinaaminika kuhusika katika kutengeneza Pombe kali bila ya kufuata taratibu.
Anayedaiwa kuwa mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho akitoa maelezo kwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Hamisi Issah pamoja na Meneja Msaidizi wa TRA Kilimanjaro anayeshughulikia masuala ya forodha ,Godfrey Kitundu ndani ya kiwanda hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...