Mbio
za Rock City Marathon msimu wa tisa zinatarajiwa kufanyika kesho jijini
Mwanza. Maandalizi ya mbio hizo zinazotarajiwa kuanzia kwenye Daraja la
Furahisha na kuishia kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini humo
yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (3,000) kutoka ndani na
nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.
Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 3,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.
“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.
Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati)
akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa
washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni
pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia)
na Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK
Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga
ndio

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi
(katikati) akionesha baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo
zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza.
Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo
akizungumza kuhusu maandalizi ya mbio hizo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...